Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo ametembelea jengo jipya la ofisi ya udhibiti ubora wa Shule Jijini Arusha iliyopo Kata ya Moshono katika ziara yake ya kutembelea miradi iliyofanyika tarehe 5-7 Novemba 2019.
Katika ziara hiyo Mhe.Gambo aliambatana na mwenyeji wake mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Mhe.Gbriel Daqarro, kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg. Sifael Kulanga, viongozi wa kisiasa wa chama cha mapinduzi ngazi ya mkoa na wilaya pamoja na wataalamu wa Jiji la Arusha.
Akizungumza katika ziara hiyo kaimu mkuu udhibiti ubora wa Elimu kanda ya Kaskazini Magharibi Bw. Festus Stephano amesema ofisi za udhibiti ubora zipo 100 hapa Nchini na katika mkoa wa Arusha zipo ofisi nne katika Halmashauri nne ikiwemo Jiji la Arusha.
Jengo hilo ambalo limegharimu zaidi ya shilingi million 152 za kitanzania kutoka serikali kuu na ujenzi wake ulianza mwezi Juni mwaka 2019 na kumalizika mwezi Oktoba 2019 ambapo mkuu wa mkoa amekagua na kuridhishwa na ujenzi huo kwani umezingatia viwango vinavyohitajika.
Mkuu wa mkoa wa Arusha amempongeza waziri wa elimu Prof. Joyce Ndalichako kwa kusimamia vizuri wizara ya Elimu.
“Nimshukuru kwa kuhakikisha kwamba maswala ya Elimu kwenye kudhibiti ubora wa Elimu yanakwenda sawa ” alisema Gambo.
Gambo amemshukuru Mhe Rais wa Jamuhuri ya muungano waTanzania kwa kujikita kwenye mpango wa Elimu nakusema pamoja na kuanzisha utaratibu wa Elimu bure nchini, ametoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za udhibiti ubora wa Elimu katika mkoa wa Arusha.
“Lengo la Mhe. Rais ni kila mtoto aende shule lakini apate Elimu iliyo bora kwa kuzijengea uwezo taasisi ambazo zinasimamia ubora wa Elimu alisema mkuu wa mkoa wa Arusha”.
Mwisho.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa