Kaya 13 zenye jumla ya wanafamilia 30 zimekumbwa na janga la moto katika Kata ya Sinoni ambapo paka sasa chanzo cha moto huo hakijafahamika hivyo kupelekea kaya hizo kupeteza mali zao na kukimbia makazi waliyokuwa wanaishi.
Pamoja na moto huo kuzuka siku ya jana muda wa saa sita za usiku imeripotiwa kutokuwepo kwa vifo wala majeruhi katika ajali hiyo ya moto isipokuwa kuteketea kwa mali za Kaya hizo.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe.Gabriel Daqarro ametoa salamu za pole kwa wote waliopatwa na janga hilo lakini pia aliambatana na wadau mbalimbali waliojitokeza kupeleka misaada ya magodoro pamoja na vyakula kwa wahanga wa moto. Wadau hao wakiwa ni kutoka kampuni ya magodoro Super Banko na Tanform walio toa jumla ya magodoro 25 pamoja na Chama cha mapinduzi ngazi ya Wilaya ya Arusha waliotoa sukari,unga,mafuta,mchele na sabuni.
Mhe.Gabriel Daqarro ameshukuru Jeshi la polisi la zima moto kwa juhudi walizoonyesha za kuzima moto eneo lile pamoja na wadau waliojitokeza kutoa misaada kwa kaya ziliyo athirika na moto huo.
Akizungumza na waandishi wa habari Mhe.Daqarro ameeleza kuwa yupo katika eneo hilo la Kata ya Sinoni akiwakilisha serikali ya awamu ya tano ambayo inajali na kuzingatia usalama wa wananchi wake hivyo wananchi wajue ya kuwa Serikali inatambua na ipo macho kuona pale wanapo hitaji msaada.
pichani:Katibu mwenezi Wilaya ya Arusha Ndg. Abraham Mollel akikabidhi msaada wa vyakula kwa wahanga wa moto
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa