Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Mhe. Gabriel Daqarro afungua semina ya mafunzo kwa wakuu wa shule za Sekondari za Wilaya ya Arusha yaliyokuwa yakiendeshwa na wakala wa maendeleo ya uongozi wa elimu (ADEM) leo Tarehe 25/09/2019.
Awali kabla ya Mkuu wa Wilaya kufungua mafunzo hayo Afisa elimu Sekondari wa Jiji la Arusha Mw.Valentine Makuka alisema lengo la kufanyika kwa mafunzo hayo ni kuwawezesha wakuu wa shule wapya na wazamani kupata mbinu mpya zakuongoza shule ambazo zitaimarisha usimamizi na utoaji wa elimu katika Jiji la Arusha. Jumla ya wakuu wa shule 32 wamehudhuria mafunzo hayo.
Katika ufunguzi huo Mhe.Daqarro alielekeza mambo muhimu kwa wakuu wa shule ambayo nimuhimu kuzingatiwa ili kuleta matokeo chanya katika tasnia ya elimu katika Wilaya ya Arusha.
Daqarro ameelekeza kuwepo na zoezi madhubuti la kudhibiti utoro wa wanafunzi mashuleni, hii nikuzingatia hasa hatua gani zichukuliwe ili kukabiliana na tabia ya utoro mashuleni. Walimu kutofumbia macho mabadiliko hasi ya tabia za wanafunzi mashuleni ikiwa hasa ni mahusiano ya baina ya wanafunzi kwa wanafunzi au wanafunzi na walimu mashuleni .
Vilevile amesisitiza kuzingatia ufuatiliaji makini wa fedha za elimu bila malipo zinazoletwa mashuleni kutoka Serikali kuu pamoja nakutoa agizo kila mwalimu afanye ukaguzi kuhakikisha hakuna fedha ilinayolipwa kwa wanafunzi hewa.
“Mkuu wa shule nae ni muwakilishi wa Serikali katika shule yake anayosimamia hivyo naomba mnapo kalia viti vyenu mkaitafasiri vyema miongozo ya Serikali” alisema Mhe. Daqarro
Lakini pia Mhe Daqarro ameelekeza walimu kupewa ushirikiano. Mwalimu apewe nafasi ya kujieleza na kusikilizwa na pia kujengewa uwezo pamoja na kuaminiwa. Rai hii imetolewa ili kuwapa vipaumbele walimu pale wanapokuwa na kero zao hivyo kupelekea utatuzi wa kero zao.
Mafunzo hayo ya sikutatu yametayarishwa kwa ushirikiano baina ya Halmashauri ya jiji la Arusha na wakala wa elimu ADEM.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa