Mkuu wa Wilaya ya ARUSHA Mhe. Said Mtanda amesema kuwa miradi saba yenye thamani ya Sh. bilioni 2.7 fedha kutoka Serikali kuu, Sh. Milioni 200 fedha za mchango wa Jiji la Arusha na Sh. Milioni 445.7 fedha kutoka Sekta binafsi itazinduliwa na mwenge wa uhuru katika Jiji la Arusha.
Mhe Mtanda ameyasema hayo leo Juni 20, 2022 alipokuwa anaongea na waandishi wa Habari kuelekea Ujio wa Mwenge wa Uhuru na Waandishi ambapo Mwenge huo utazindua mradi wa Maji uliofadhiliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWSA ) katika Zahanati ya Terrat ambapo mamlaka hiyo imeweka kizimba maalum cha maji kilichoboreshwa.
Akizungumza na wandishi wa Habari juu ya ujio wa mwenge huo Jijini Arusha, Mhe. Mtanda alisema mwenge huo utaweka jiwe la msingi mradi wa Afya kituo Cha Afya cha mkonoo sanjari na ukaguzi wa warahibu(soba house)eneo la Njiro
"Nawakaribisha wananchi wote wafike katika maeneo tofauti ambayo mwenge utakwenda kuzindua miradi hii,pia na mwenge huu utafika Jiji la Arusha Juni 22 na utapokelewa Viwanja vya Magereza ukitokea Wilayani Monduli na Jiji tutaukimbiza kwa siku moja, hivyo wananchi wajitokeze kwa wingi"
Alisema pia utazindua barabara ya Themi viwandani eneo katika mradi wa kutengeneza chakula cha mifugo sanjari na kutembelea mradi wenye kuongezea thamani za mazao ya nyuki eneo la nanenane.
Baada ya uzinduzi huo mwenge huo utakesha eneo la viwanja vya Kilombero ambapo kutakuwa na taarifa mbalimbali na risala ya utii kwa Rais, Samia Hassan Suluhu itasomwa ikiwemo burudani katika vikundina wasanii mbalimbali.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa