Ametoa rai hiyo mbele ya Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dr. Maulid Suleiman Madeni wakati alipotembelea ofisi za makao makuu ya jiji leo Tarehe 11/10/2018 kwa ajili ya kumsalimia mkurugenzi huyo pamoja kumjulisha juu ya mpango wa ziara ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha katika Jiji hili kwa ajili ya kukagua thamani ya fedha katika miradi ya wananchi iliyoanzishwa na kusimamia utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Mwenyekiti huyo amempongeza Dr. Madeni kwa opereseni yake ukusanyaji wa mapato aliyoianzisha kwani anaamini mapato hayo yanakwenda kusaidia kuboresha huduma za wananchi na ameelezea mikakati ya ziara za chama kuzitembelea Halmashauri zote katika Mkoa wa Arusha ikiwemo Halmashauri ya Jiji kuhakikisha miradi iliyoanzishwa inatekelezeka kikamilifu kwa ajili ya kuwasaidia wananchi.
“ Miongoni Mwa makosa yaliyofanywa na viongozi wa chama kipindi cha nyuma ni kuwaachia watendaji wa serikali peke yao katika kusimamia miradi ya wananchi matokeo yake wanapotokea watendaji wasio waadilifu tunakwama kiutendaji pindi tunapoenda kukukatana na wa wananchi kwani tumeshindwa kutekeleza ahadi tulizowapa” alisema Mhe. Sannare
“Sisi kama chama hatutavumilia kuona kiongozi yoyote wa serikali anakwamisha jitihada za mwenyekiti wetu wa chama cha cha mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli katika kutekeleza ahadi za kwa wanachi, tutahakikisha tunapita kila uchochoro kunatatua changamoto zote zinazowakabili ” aliongeza mwenyekiti huyo
Naye mkurugenzi wa jiji la Arusha Dr. Maulid Suleiman Madeni alimshukuru Mhe. Sannare kwa kumtembelea na kumuahidi kuwasimia vizuri watendaji walio chini yake katika kuhakisha shughuli zinazotekelezwa katika halmashauri yake zinakuwa chachu kwa wananchi hasa wa hali ya chini.
“Agenda kubwa iliyopo katika nchi yetu sasa hivi ni ukusanyaji wa mapato, nichukue fursa hii kukuomba wewe pamoja na viongozi wengine wa vyama tushirikiane kuwahamasisha wananchi juu ya umuhimu wa kodi, na itapendeza katika operesheni zangu za ukusanyaji wa mapato ninazoziendesha niwe naambatana na viongozi wa vyama vyote katika kuhamasisha ulipaji wa kodi na ukusanyaji wa ushuru kwani maendeleo ya wananchi wetu hayangalii itikadi za dini wala za vyama vya siasa ” Alisema Dr. Madeni
Dr. Madeni aliongeza kwa kusema kuwa yupo tayari kwa ziara ya chama katika halmashauri yake na kuahidi kutoa ushirikiano wa hali na mali katika kuhakikisha zoezi linafanikiwa kwa maslahi ya wananchi.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa