Na Mwandishi Wetu
Baraza la Madiwani wa Jiji la Arusha limemchagua, Diwani wa Viti Maalum (CCM), Veronica Mwelange kuwa Naibu Meya wa Jiji hilo ambaye amepata kura zote 32 zilizopigwa na madiwani hao.
Akizungumza leo Alhamisi Julai 28, 2022 katika kikao hicho cha Baraza la Madiwani, Meya wa Jiji la Arusha, Maximilian Iranqhe amesema kuwa, Naibu Meya amepita baada ya jina lake kupita bila kupingwa.
Mhe. Iranqhe amesema kuwa, Veronica amefanikiwa kutetea nafasi yake baada ya kuongoza nafasi hiyo tangu mwaka 2020.
Kwa upande wake Naibu Meya huyo amesema kuwa kama ilivyo mwaka mpya wa fedha mambo yawe mapya huku akiwataka madiwani kuunganisha nguvu kujenga halmashauri hiyo.
"Mwaka uliopita yawezekana wengine tulikuwa wageni ila tumejifunza mengi na sasa tunaenda kuijenga halmashauri yetu na kuhakikisha tunaongeza mapato na kuwa mfano bora wa kuigwa."amesema Naibu Meya.
Amesema kuwa siri ya mafanikio ya kupeta mara ya pili ni kutokuwa na makundi wala makandokando katika uongozi wake ambapo amesema atahakikisha anasimamia kwa uaminifu shughuli mbalimbali ndani ya jiji hilo.
Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii ikiwemo elimu, Afya na uchumi, Diwani wa Kata ya Ngarenaro, Isaya Doita amesema kuwa, amechaguliwa na madiwani hao baada ya kuwa na imani naye na atahakikisha anaisimamia kamati hiyo vizuri na kwa vitendo kuhakikisha wanaboresha huduma hizo ipasavyo.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa