Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Mwita Waitara amefanya ziara Jijini Arusha mapema leo Tarehe 8 Januari 2020 kutembelea shule ya Sekondari ya Mrisho Gambo iliyopo Kata ya Olasiti akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo, Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro, pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Dkt. Maulid Madeni.
Akizungumza katika ghafla hiyo Mhe. Mwita Waitara amepongeza uongozi wa Mkoa, Wilaya pamoja na Halmashauri kwa umoja wa kusimamia na kuendeleza vyema miradi ya maendeleo hususani katika sekta ya elimu Jijini Arusha. Pia amewapongeza wadau wote waliotoa mchango katika ujenzi wa shule hiyo kwani kwa kufanya hivyo wamemuuga mkono Mhe. Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika kuimarisha Sekta ya Elimu hapa nchini.
Mhe. Waitara amesema kwa niaba ya Serikali amefurahishwa na kitendo cha zaidi ya Wanafunzi 4000 wa kidato cha kwanza katika Mkoa wa Arusha waliokua na ukosefu wa vyumba vya madarasa kufanikiwa kuanza masomo kwa muda, ambapo paka kufikia Tarehe 6 Januari 2020 wote walianza masomo.
Hata hivyo Mhe. Waitara amewaagiza TARURA ngazi ya Mkoa na Wilaya kurekebisha barabara ya kuingia shule hiyo ili kurahisisha usafiri kwa wanafunzi na Walimu kwani shule hiyo imejengwa kwa gharama kubwa na kwa kuzingatia ubora wa hali ya juu hivyo miundo mbinu pia iwe ya kuridhisha.
Pia Mkuu wa Mkoa Mhe. Mrisho Gambo amemalizia kwa kusema kua ataendelea kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Arusha katika harakati za kujenga mabweni ya shule hiyo pia ameeleza kuwa serikali imeelekeza nguvu katika kuzalisha Wanasayansi wengi zaidi hivyo watu wasidhani kwamba shule bora ni Shule za binafsi tu bali pia kwa upande wa Serikali kuna shule nzuri ikiwemo Shule ya Sekondari ya Mrisho Gambo amesisitiza kua shule hiyo siyo ya Mkoa bali ni ya Halmashauri ya Jiji la Arusha.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa