Naibu Waziri afurahishwa na Umoja Viongozi Arusha,asifu Bonanza
Na Mwandishi wetu
Naibu Waziri Habari ,Sanaa na utamaduni na Michezo Mh. Abdallah Ulega ameeleza kufurahishwa na umoja wa Viongozi wa Mkoa wa Arusha na wananchi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa kuungana kushiriki Michezo na Bonanza .
Wananchi hao wameungana pamoja kushiriki Michezo iliyoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Kenan Kihongosi kwa kushirikiana na viongozi wenzake na wadau wa Michezo .
Mh.Ulega amesema kuwa suala la michezo lipo kwa mujibu wa ilani ya Chama cha mapinduzi imeagiza wa Viongozi katika Tawala za Mikoa waweze kuandaa mabonanza ikiwa ni kuwaletea watanzania pamoja na kwamba Arusha wamevunja rekodi .
Amewataka Viongozi wa Arusha kuendelea na umoja huo kwa faida ya maendeleo ya wakazi wa Arusha na kupuuza watu wenye kubeza umoja jitihada hizo .
Mkuu wa Mkoa Arusha Mh.Idd Kimanta akizungumzia Michezo hiyo amesema kuwa Viongozi wa Arusha wanatekeleza maagizo ya Viongozi wa juu serikalini pamoja na Ilani ya Chama cha Mapinduzi inayohimiza Michezo ikiwa ni kujenga umoja.
Alisema wakazi wa Mkoa wa Arusha na Viongozi wameungana kwa pamoja kuijenga Arusha na kwamba njia mojawapo yakuungana ni kupitia Michezo .
Kwa upande wake ,Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mh.Kenan Kihongosi akizungumzia Michezo na Bonanza hilo ameshukuru wadau wa Michezo na Wananchi wa Arusha kushiriki kwa wingi katika Michezo na Bonanza hilo .
Anasema kuwa Michezo hiyo ni endelevu nakuwa nia ni kuibua vipaji vya wachezaji wa Michezo mbali mbali na hatimaye kuwawezesha kupata ajira kupitia vipaji vyao .
Meya wa Jiji la Arusha Maximilian Iraghe na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Dk.John Pima wakizungumza katika Bonanza hilo ,walisema kuwa jukumu lao kama Viongozi ni kuwaletea Wananchi maendeleo na kwamba Michezo ni miongoni mwa vitu vinavyoleta maendeleo .
Wanasema kuwa Arusha kwa sasa ni kazi na kuwa wamepania kuwaletea wananchi maendeleo kwamba Michezo ni mwanzo wa kuonyesha nia njema ya kuletea wananchi maendeleo .
Bonanza hilo lina Michezo 24 ikiwa na mpira wa miguu unaoshirikisha timu ya washabiki wa Simba na Yanga na washindi watazawadiwa Ng'ombe na kupewa medali za ushindi na Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Abdallah Ulega.
MATUKIO KATIKA PICHA YANAONESHA UHALISIA WA WASHIRIKI WA BONANZA NA MICHEZO WAKIWA KATIKA PICHA WAKATI WAKICHEZA NA BAADA YA KUMALIZA MAZOEZI YA KUKIMBIA NA KUCHEZA
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa