Mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji la Arusha Mhandisi Juma Hamsini amesema wenyeviti wa mitaa 154 wapo kwenye utaratibu wakulipwa posho zao za 100,000 kila mwezi kama ilivyokubalika awali.
Kauli hiyo ameitoa alipokuwa akijibu swali la Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella walipokuwa wakikagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Jiji hilo.
Juma Hamsini amesema malipo ya wenyeviti hao yalichelewa kutokana na kutowekwa kwenye bajeti ya mwaka 2023/2024 lakini kutokana na uzito wake halmshauri ya Jiji la Arusha lilitambua hilo na litafanya mabadiliko madogo ya bajeti yake ifikapo Disemba ili kuweza kupata fedha hizo na watalipwa mapema.
Amesema watendaji hao wamekuwa ni msaada mkubwa kwa Jiji kwani waliweza kuainisha vyanzo mbalimbali vya mapato katika maeneo yao.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi Juma Hamsini ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuleta fedha nyingi za miradi ya maendeleo katika Jiji hilo na kuwezesha kuwa na miradi yenye tija na itakayoleta maendeleo kwa wananchi.
Ziara ya Mkuu wa Mkoa ya kukagua miradi ya maendeleo katika Jiji la Arusha itafanyika kwa siku mbili na miradi itakayopitiwa ni afya, elimu barabara hasa za mradi wa TACTIC na Maji.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa