Afisa Mifugo wa Jiji la Arusha Dkt. Onesmo Mandike leo Tarehe 23/09/2019 amefanya oparesheni ya ukamataji wa mbwa wanao zurura mtaani wasiokuwa na makazi maalumu na kuwapatia chanjo ya kichaa cha mbwa pamoja na kuwafunga uzazi/kuhasi.
Zoezi hili limeandaliwa kwa malengo ya kupunguza idadi ya mbwa wanao zagaa mtaani na kusababisha kero kwa jamii lakini pia kutokomeza maambukizi ya kichaa cha mbwa kwa binadamu.
Kwa muda mrefu Jiji la Arusha limekumbwa na tatizo la kuwa na mbwa wengi wanaozurura kwenye mitaa, mbwa wasio na mkazi maalumu hivyo kupelekea kuwa kero kubwa katika jamii hususani maeneo yenye idadi ya wakazi wengi. Mbwa wa mtaani wamekuwa kero haswa pale wanapowajeruhi binadamu.
Oparesheni hii imeanzishwa ili kupunguza athari zinazoweza kutokea pale mbwa anapo ng'ata binadamu lakini pia opereshen hii inasaidia kudhibiti kuzaliana kwa mbwa hivyo kupelekea mbwa wazururaji kuongezeka.
Takribani mbwa 1637 wamehasiwa katika Jiji la Arusha na Kata zilizofikiwa na zoezi hili ni Kimandolu, Baraa, Oloirien, Sekei, Lemara na Daraja II.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa