Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amesema serikali itaendelela kuliimarisha Jeshi la polisi kwa kuboresha miundombinu, vitendea kazi na maslahi ya Askari na kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unakuwepo wakati wote.
Rais amemwagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simo Siro kuhakikisha askari wanatumia mbinu za kisasa kukabiliana na kilimo cha bangi na kuacha mara moja kwenda kufyeka na kuchoma mashamba ya bangi.
Ameyasema hayo alipokuwa akihutubia maelfu ya wananchi baada ya ghafla ya uzinduzi wa nyumba 31 za polisi, kituo cha utalii na kushuhudia mazoezi ya askari polisi kukabiliana na wahalifu katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliopo jijini hapa.
Rais Magufuli ametoa shilingi bilioni 10 kwa ajili ya kuboresha makazi ya polisi kote nchini na pia amewapongeza viongozi wa mkoa wa Arusha kwa kuwashirikisha wananchi wakiwemo wawekezaji kufanikisha ujenzi wa nyumba hizo.
Mkuu wa jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Siro na Waziri wa Mambo ya Ndani nchini. Mhe. Mwigulu Nchemba pamoja na kumweleza Rais baadhi ya changamoto zinazolikumba jeshi la polisi nchini wamesema wanaendelea kuzikabili kwa kuimarisha vikosi vya doria usiku na mchana.
MWISHO.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa