RC Arusha adai anaheshimu mawazo ya kila mtu, afurahishwa na kampeni ya Usafi
Na Mwandishi wetu
Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella amesema kuwa anaheshimu mawazo ya kila mtu kwa kuamini kuwa hakuna mtu mwenye akili timamu asiyekuwa na wazo la kujenga.
Mh.Mongella amewataka wananchi wenye mawazo ya namna yakujenga Mkoa wa Arusha na Halmashauri zao kumshirikisha.
Akizungumza wa wadau wa maendeleo ya Utalii, wananchi wa Jiji la Arusha ,Viongozi wa Jiji la Arusha, wakati wa zoezi la usafi mlima Suye alieleza kufurahishwa na kampeni ya usafi kwenye vivutio vya Utalii ikiwemo Mlima Suye kampeni inayoongozwa na Meya ya Jiji la Arusha pamoja na Wataalam wa Halmashauri ya Jiji la Arusha chini ya usimamizi wa Dk.John Pima.
Mh.Mongella alisema kuwa Jiji la Arusha linakwenda kuwa mfano wa usafi na kutunza mazingira na kwamba mawazo ya wadau ni muhimu katika kuboresha vivutio vya Utalii.
Mh.Mongella alisema kuwa anaamini katika Umoja na mshikamano kuwa amebaini Arusha kuna mshikamano na Umoja na kwamba kiongozi atakayejitenga atatafutwa aje aungane na wengine katika Umoja.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mh.Kenan Kihongosi alimshukuru Mkuu wa Mkoa pamoja na kumpongeza Meya wa Jiji la Arusha pamoja na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha kwa kuanzisha kampeni hiyo yenye manufaa kwa maendeleo.
Meya wa Jiji la Arusha Maximilian Iranqhe alisema kuwa zoezi la usafi katika Jiji la Arusha ni endelevu kwamba baada yakumaliza kufanya usafi katika vivutio vya kitalii sasa watakwenda kufanya katika masoko yaliyopo Jiji la Arusha.
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dk.John Pima akielezea kampeni hiyo alisema kuwa Halmashauri ya Jiji la Arusha ina mipango kabambe yakuboresha miundo mbinu katika maeneo yenye vivutio vya Kitalii.
Alisema Mlima Suye ni miongoni mwa vivutio vitakavyowekewa miundo mbinu ikiwa ni kuwezesha watu kupanda kwa urahisi hadi KiIeleni.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha pia alipanda miti ikiwa ni ishara ya Utunzaji na uhifadhi wa mazingira katika Mlima Suye.
PICHANI : Matukio mbalimbali katika picha kwenye zoezi la kampeni ya Usafi inayoendelea Jijini Arusha ambapo viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Arusha wakiwemo Mkuu wa Mkoa Ndg. John Mongella, Mkuu wa Wilaya Mh.Kihongosi, Mstahiki Meya Mh. Maximilian Iranqhe, Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt John Pima na wadau mbalimbali wa maendeleo waliweza kushiriki.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa