Na Mwandishi wetu
Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella amesema kuwa Sauti ya pamoja ya Viongozi katika mambo ya msingi ya maendeleo katika Mkoa wa Arusha itakuwa ni agenda namba moja.
Mh. Mongella alisema Umoja na sauti ya pamoja itawezesha kukusanya mapato kutoka vyanzo vyote vya mapato na kubuni vyanzo vipya vya mapato ikiwa nikuwezesha kuendeleza miradi ya maendeleo katika Halmashauri husika.
Mh.Mongella akizungumza na Viongozi na wadau wa maendeleo katika Halmashauri ya Jiji la Arusha mara baada yakumaliza ziara ya kuzuru miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Jiji la Arusha alisema ameridhika na miradi ya maendeleo aliyotembelea na kudai kuwa ili kuendeleza kutelekeza miradi kama hiyo lazima Viongozi wawe na sauti ya pamoja katika kukusanya mapato katika vyanzo husika.
Alisema kuwa suala utoaji mapato halina mjadala kwa kuwa maendeleo yanategemea mapato nakutaka wananchi kutekeleza wajibu wao kulipa kodi kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mh.Kenan Kihongosi na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dk.John Pima wakizungumza kwa nyakati tofauti walisema ukusanyaji wa mapato ni agenda namba moja nakumhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa wataendelea kuhimiza ukusanyaji wa mapato.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh.John Mongella ametembelea miradi mbali mbali ya Halmashauri ya Jiji la Arusha ikiwemo hospitali ya Wilaya ya Arusha.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa