Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongela amewapongeza viongozi wa Jiji la Arusha kwa ujumla, Wananchi na Machinga kwa kushirikiana kwa pamoja katika kukamilisha zoezi la uhamaji wa machinga kutoka sehemu zisizo rasmi kwenda katika sehemu rasmi za kufanyia biashara.
RC Mongela ameyasema hayo hii leo Tarehe 20 Nov 2021 alipokua akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha wakiwemo wakuu wa idara, Watendaji wa Kata na Mitaa pamoja na viongozi wa Machinga wa Wilaya ya Arusha.
Sambamba na pongezi hizo, RC Mongela amewaonya viongozi wa Jiji la Arusha wote kwa vyeo vyao kutowabughudhi wamachinga kwa kuwatoza fedha za Ushuru wala Pango kwani utaratibu huo haupo isipokua machinga watawajibika kulipa fedha za umeme, maji na ulinzi kulingana na vile watakavyo kubaliana.
"Jana nimesikia eti Kuna mtu Pale namba 68 anawatoza wamachinga shilingi 500 ya ushuru kwa siku, tafadhal akitokea mtu anataka kutoza kodi katika maeneo haya tuliyo yaandaa hatutakubali... hakuna eneo tulilojenga kwaajili ya kupangisha. Kwa taarifa ambazo sijazithibitisha, katika Safu za utendaji wetu Kuna wachawi, wanataka kujinifuisha kupitia michezo hiyo tukimfahamu imekula kwake" RC John Mongela.
Aidha RC Mongela amekiri kuwepo kwa changamoto ndogondogo katika maeneo mapya walikohamia wafanyashara hao lakini amewataka wafanya biashara hao kuendelea kuvumilia changamoto hizo kwani siku zinavyozidi kwenda biashara zitazoeleka na kuimarika.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa