Na Mwandishi Wetu, Arusha
MKUU wa Mkoa Arusha Arusha, Mhe. John Mongella amewaagiza wakufunzi wa sensa na watu na makazi ngazi ya Mkoa, kuhakikisha wanachukua takwimu sahihi ngazi ya kaya ili kuwezesha serikali kupa ta mipango ya maendeleo kulingana na takwimu sahihi zitakazopatikana.
Pia amewataka kila mmoja kutanguliza uzalendo na weledi katika kazi hiyo na kila mmoja alichukulie kwa uzito wanaostahili kwani linaenda tengeneza njia inayostahili.
Akizungumza leo Jijini Arusha wakati akifunga mafunzo ya wakufunzi wa sensa ya watu na makazi ngazi ya Mkoa yaliyofanyika kwa wiki tatu,Mongella amesisitiza uzalendo katika kazi hiyo sababu ndio msingi wa ufanisi wa kazi hiyo.
"kuweni wazalendo katika zoezi hilo sababu mtapewa vifaa kama vishikwambi mvitunze hii ni mali ya serikali msilete sababu kuweni na umakini wa utunzaji vifaa hivi ili msipoteze amani nahisi serikal mtatupotezea amani kuwa zoezi katika eneo hili halitakamilika kwa wakati,".
Alisema zoezi lifanyike kwa umakini na liishe ndani ya muda,ili kuleta sifa inayostahili ndani ya mkoa huo.
"Tangulizeni uzalendo katika kazi hii ni muhimu sababu serikali imetoa fedha nyingi kukamilisha kazi hii,hivyo umakini uwe mkubwa na nyie ndio inawategemea kufanikisha zoezi la sensa kwa umakini mkubwa,"
Aidha alisema serikali inafanya masuala mengi ya maendeleo na kupata sifa nyingi,lakini zikipatikana takwimu sahihi maendeleo yatafanyika zaidi ya sasa kulingana na takwimu sahihi zitakaopatikana.
"Kila mtu ana nafasi yake na anatakiwa kufanya kitu kwa nchi msijidharau nafasi hii mmepata ya kihistoria kwenu nanyi simamieni kuhakikisha inasaidia serikali kwa kufanya kazi vizuri,.
Naye Mkufunzi Mkuu wa mafunzo hayo, Mdoka Omari alisema jumla ya wakufunzi 15wamepata mafunzo ngazi ya Taifa kwa siku 21 mkoani Iringa na ngazi ya Mkoa kwa wiki tatu.
"Lakini hapa katika mafunzo yetu jumla ya watumishi 329 kutoka Halmashauri zote za mkoa huu,kundi la watu wenye ulemavu na baadhi ya Taasisi zinazoshirikiana na serikali katika masuala ya sensa,"alisema.
Alisema washiriki alipewa majaribu ya kuwapima ili kuona tayari wao wqtakapokwenda ngazi za kata kutekeleza majukumu yao na walifanya vizuri.
Naye mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Athumani Kihamia ambaye ni Ofisa Mipango Mkoa wa Arusha , Said Mabiye alisema wanataraji sensa ya watu nanmakazi itawasaidia kupata takwimu sahihi.
Alisema upatikanaji wa takwimu sahihi kunawezesha upangaji wa mipango ya maendeleo kulingana na idadi halisi.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa