Na Mwandishi Wetu
Arusha.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella amekemea uwepo wa vitendo vya ulawiti na ushoga nakubainisha kuwa endapo watabaini Taasisi yoyote inayojihusisha na Ushoga au mtu yoyote hawatamvumilia na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Mhe. Mongella ametoa wito huo leo Aprili 20, 2023 wakati akizindua Wiki ya Maadhimisho ya miaka 59 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar kimkoa yaliyokwenda sambamba na Uzinduzi wa vyumba vinne vya madarasa katika Shule ya sekondari kaloleni.
Mongela amesema kumekuwa na tetesi za uwepo wa Taasisi zinazojihusisha na kutoa elimu ya vitendo vya ushoga, usagaji na ulawiti na kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama kufuatilia Taasisi hizo pamoja na Kuwataka wanafunzi kuripoti taarifa za ushoga pindi wanapokutana nazo wawapo Shuleni au majumbani.
"Kuna watu wanatajwa Arusha Kuna Taasisi Mimi vyombo vya ulinzi na usalama nilishatoa maelekezo Taasisi hizi tuzifatilie hakuna mtu ataonewa Wala kunyanyaswa Ila ukithibitika nitakushughulikia alisema Mongella "
Aidha amesema Serikali imeweka mkazo kwenye elimu na inapambana kupata vijana bora ili kuwa na Taifa endelevu na kuwataka Wanafunzi kuzingatia elimu na kuongeza kuwa kuwekeza kwenye elimu kutasaidia kuwa na Taifa bora zaidi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Felician Mtahengerwa alisema hali ya ulawiti na ushoga ni mbaya sana na kuwaomba walimu kuwasaidia mashuleni kuwa pasiwepo na Taasisi yoyote inayoenda kufundisha mashuleni bila uongozi wa Wilaya kuwa na taarifa kwani kumekuwepo na Taasisi zinaenda kwa lengo lingine ambalo limejificha.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Bw. Hargeney Chitukuro akitoa taarifa ya mradi wa madarasa manne katika Shule ya sekondari kaloleni amesema mradi huo ulianza October 28 ,2022 na unathamani ya shilingi milioni 80 ukiwa na viti na meza.
"Mradi huu ulianza baada ya kupokea fedha kiasi cha Shilingi milioni 80 kutoka Serikali kuu lengo likiwa ni kupunguza uhaba wa madarasa ili wanafunzi watakao ingia sekondari mwaka huu 2023 waweze wote kuingia darasani na lengo limetimia madarasa hayo yamekamilika na yanatumika ,alisema Chitukuro"
Naye shukuru Daniel mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya sekondari kaloleni ameishukuru serikali kwa kuwajengea vyumba vya madarasa Shuleni hapo na kuahidi kusoma kwa bidii ili waweze kusaidia nchi kuweza kuendelea kiuchumi katika sekta mbali mbali.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa