Kufuatia maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa Tanzania bara kwa Ngazi ya Mkoa yaliyo fanyika 8/12/2021 katika kiwanja cha Makumbusho Jijini Arusha, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella amewataka Walimu, Maafisa Elimu na Viongozi kutilia mkazo somo la historia ili wanafunzi wa Kitanzania wafahamu Nchi ilikotoka ili wasiwe chanzo cha kuiyumbisha.
Mhe. Mongella ambaye pia ndiye Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo ameyasema hayo alipokua akihutubia hadhara iliyo hudhuria katika maadhimisho ya uhuru wa Tanzania bara ngazi ya Mkoa ikiwa ni agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ili 9/12/2021 Watanzania wote wapate furusa ya kushiriki ama kufuatilia maadhimisho ya kitaifa.
Mhe. Mongella anasema " Ujumbe wangu kwenye Shule zetu, Maafisa Elimu, Walimu na sisi Viongozi tusisitize somo la Historia, mtu asiyejua alikotoka, alipo huyo mtu hana uelekeo na iko siku wataleta vurugu"
Kwa upande mwingine amewataka Watanzania wote kuendelea kuitunza, kuenzi misingi iliyoachwa na Muasisi wa Taifa la Tanzania, kuzilinda Tunu za taifa la Tanzania ambazo ameziorodhesha kama Amani, Usalama na Mshikamano.
Kadhalika Spika wa Bunge la Jumuiya ya Africa Mashariki ambaye pia ni Mgeni Maalum Katika tukio hilo Mhe. Mathias Ngoga amewapongeza Watanzania kwa kufikisha miaka 60 ya uhuru na kuwasisitiza kuitunza na kuilinda amani ya Nchi kwani huo ndio msingi wa mafanikio katika nyanja zote za maisha.
Akiitolea mfano Nchi yake ya Rwanda ambayo imewahi kuingia katika machachafuko ya vita za wenyewe kwa wenyewe, amewasisitiza Watanzania kutojenga mazoea na amani yao na kuona ni kitu cha kawaida kwani pale inapopotea inagharama kubwa kuirudisha.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa