Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji ka Arusha Athumani Kihamia ametakia kheri wanafunzi wa kidato cha Sita wanaoendelea kufanya mitihani katika shule mbalimbali zilizoko katika Jiji hilo.
Akizungumza Ofisini kwake Kihamia amesema Watahiniwa wa kidato cha sita wanaoendelea na mitihani katika Jiji hilo ni 805 kati yao Wavulana ni 416 na wasichana 389.
Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Valentini Makuka amesema kuwa miongoni mwa watahiniwa hao (School Candidate) ni 605 ambapo wavulana ni 296 na wasichana ni 309 na Watahiniwa wa kujitegemea (Private candidate) wanaofanya mtihani wa kidato cha sita ni 200; Wavulana ni 107 na wasichana ni 93.
Makuka amevitaja vituo vya kufanyia mitihani vipo 6 na wanafunzi wanaendelea kufanya mitihani pasipo kuwa na changamoto yoyote.
"Mitihani inaendelea vizuri na Hadi sasa hakuna changamoto yoyote kubwa iliyojitokeza wakati mitihani ikiendelea". alisema.
Ameongeza kuwa anaamini wanafunzi watafanya vizuri kwa kuwa wameandaliwa vizuri na walimu wao na wao wamefanya mazoezi ya kutosha.
Mtihani wa Taifa wa kidato cha sita umeanza Mei 7, 2018 na unahusisha shule mbalimbali za sekondari nchini kote zikiwemo za Serikali na za binafsi.
Kamati ya mitihani ya Jiji la Arusha pia inasimamia watahiniwa wa mafunzo ya ualimu ambao wanafanya mitihani ya cheti cha ualimu cha daraja la IIIA. Watahiniwa hao wa mafunzo ya ualimu wapo 158 wakiume 81 na wakike wakiwa 77.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa