Pichani: Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Said Mtanda akikabidhi kishikwambi kwa mmoja wa Walimu wa Jiji la Arusha.
Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia leo Januari 10,2023 imekabidhi jumla ya vishikwambi 1659 vilivyotumika katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi kwa makundi mbalimbali ya watumishi wa kada za Elimu Msingi na Sekondari wa Halmashauri ya Jiji la Arusha lengo likiwa ni kuboresha Sekta ya Elimu nchini.
Zoezi hilo limefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa shule ya sekondari Arusha na kuongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Said Mtanda ambapo ameyataka makundi hayo ya Elimu kuvitunza na kutumia vishikwambi hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa na si vinginevyo.
Pichani: Wataalam wa Elimu wakifuatilia jambo kwa umakini katika hafla fupi ya makabidhiano ya vishikwambi Jijini Arusha.
Ikumbukwe kuwa, serikali ilitoa tamko kuwa vishikwambi vilivyotumika kwenye Sensa ya Watu na Makazi kugawiwa walimu nchini lengo likiwa kuimarisha na kuboresha ufundishaji na ujifunzaji mashuleni.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa