Serikali yaridhishwa na miradi ya miundo mbinu Jijini Arusha.
Na Mwandishi wetu
SERIKALI imesema kuwa imeridhishwa na utekelezaji wa miradi ya miundo mbinu ya elimu na miradi mingine ya maendeleo katika Halmashauri ya Jiji la Arusha na kwamba imetekelezwa kwa viwango vinavyotakiwa kulingana na fedha zilizotolewa kwa miradi husika .
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mh .Kenan Kihongosi ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Arusha kwenye mkutano wa robo ya Pili wa Baraza la Madiwani katika Ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa.
Mh.Kenan alisema kuwa anajivunia kuona fedha za miradi zilizotolewa na Serikali ya Mh. Dk.John Pombe Magufuli na kwamba miradi imekamilika kwa asilimia 95 kwamba kukamilika kwa miradi hiyo ikiwa ni pamoja na miradi ya Elimu imewezesha wanafunzi kujiunga kidato cha kwanza bila kikwazo.
Aliendelea kwa kumpongeza Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dk. John Pima kwa kusimamia vyema fedha za Serikali na kuwezesha miradi kukamilika kwa wakati.
Pamoja na mambo mengine alisema kuwa mafanikio hayo yamepatikana kwa ushirikiano wa madiwani na wataalam na kudai kuwa Serikali inajivunia uongozi huo.
Awali Mh. Meya wa Jiji la Arusha, Maximilian Iranqhe alipongeza jitihada za Mkuu wa Wilaya ya Arusha kwa kushiriki kikamilifu katika Ujenzi wa madarasa mwaka 2020 na kwamba Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mh. Kenan Kihongosi ni mfano wa kuigwa.
Mh .Iranqhe alisema kuwa nia ya Viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha nikuwaletea Wananchi Maendeleo na kudai kuwa Arusha itakuwa mji wa mfano kwa kuwaletea wananchi maendeleo.
Mkutano huo wa Baraza unahudhuriwa na wadau mbali mbali wa maendeleo ikiwa ni pamoja na Wananchi wa Jiji la Arusha.
MATUKIO KATIKA PICHA : MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI ROBO YA PILI HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA 2021
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa