• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Arusha City Council
Arusha City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Fedha na biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Usafishaji na Mazingira
      • Works and Infrastucture
      • Water
      • Mipango, Uchumi na takwimu
      • Mipango miji
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
    • Vitengo
      • Sheria
      • Tekinolojia ya habari Mawasiliano na Mahusiano
      • Manunuzi
      • Internal Audit
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa nyuki
    • Kata
      • Baraa
      • Daraja II
      • Elerai
      • Engutoto
      • Kaloleni
      • Kati
      • Kimandolu
      • Lemara
      • Levolosi
      • Moivaro
      • Moshono
      • Murriet
      • Ngarenaro
      • Olasiti
      • Olmoti
      • Oloirien
      • Osunyai
      • Sakina
      • Sekei
      • Sinon
      • Sokon I
      • Sombetini
      • Terrat
      • Themi
      • Unga Ltd
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Usafi wa Mazingira
    • Elimu
    • Biashara
    • Maendeleo ya Jamii
    • Leseni
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe.Wabunge na Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Maadili
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba za Vikao
      • Ratiba ya kumuona Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • STUDY ONLINE
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Hotuba
    • Taarifa kwa umma

SERIKALI YASEMA HAKUNA UPUNGUFU WA CHANJO KWA WATOTO

Posted on: April 15th, 2021

Serikali yasema hakuna upungufu wa chanjo kwa Watoto 

Na Mwandishi Wetu 

Serikali imesema kuwa hakuna upungufu wa chanjo kwa akina mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano na kwamba chanjo hizo zipo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya na hospitali na kwamba zinatolewa bure bila malipo. 

Akizungumza na wataalam wa afya katika Kituo cha Afya Kaloleni Halmashauri ya Jiji la Arusha  Mkurugenzi wa Kinga  kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi amesema taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusu upungufu wa chanjo hazina uhalisia na kwamba chanjo iko ya kutosha katika vituo vyote vya kutolea huduma za Afya nchini. 

Dr. Subi alisema kuwa ni jukumu la wataalam wa Afya kuwahudumia wanawake na watoto bila kikwazo ikiwa ni njia mojawapo yakupunguza na kuondoa kabisa vifo vya akina mama na watoto nchini. 

Aliongeza kuwa kuwa Serikali ya awamu ya sita inawajali wanawake na watoto nakuwa wataalam wa Afya wanajukumu lakuhakikisha kuwa kundi hilo linapata huduma bora bila kikwazo. 

Pia aliagiza Waganga wakuu wote nchini kuhakikisha wanaweka Televisheni na vipeperushi katika vituo vya kutolea huduma za Afya hususani katika majengo wanayohudumia akina mama wajazito na kuweka vipindi vinavyoelimisha akina  mama juu  ya afua mbali mbali za Afya ya uzazi na jinsi ya kujikinga na magonjwa ya kuambukiza na yale yasiyo ya kuambukiza.

“Naagiza Waganga wakuu wote nchini kununua na kuweka Televisheni katika vituo vya kutolea huduma za Afya na hospitali ili kuwapatia fursa akina mama kujifunza afya ya uzazi ikiwa ni njia ya kupunguza vifo vya akina mama wajawazito .” alisema  Dkt. Subi.

Pamoja na mambo mengine aliwataka akina mama wajawazito kujali Afya zao kwa kuhudhuria Kliniki kwa wakati ili kupata huduma bora ikiwa ni pamoja na kulinda watoto waliopo tumboni .

“Niwaombe akina mama mjali Afya zenu pamoja na kulinda haki zenu kwa kuhakikisha kuwa hakuna mtaalam anayekuonea pindi unapofika hospitalini au vituo vya afya kwa kuwa ni haki yenu kupata huduma ya afya bila kikwazo “ anasema Dk. Subi. 

Hata hivyo alipongeza Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa huduma bora za afya kwa wananchi ikiwemo akina mama na watoto kuwa utamaduni huo unapaswa kuendelezwa ikiwa ni kuendelea kuwahimiza wanaume kusindikiza wake zao katika vituo vya afya na hosiptali .

Dr.subi alisema wanaume wanamchango mkubwa katika kuhakikisha wake zao wanajifungua salama ikiwa ni kuhakikisha kuwa wamehudhuria katika kliniki kwa wakati .

Mganga mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Dkt. Kheri Kagya alisema kuwa maagizo ya Serikali yatafanyiwa kazi na kwamba Halmashauri ya Jiji la Arusha ina chanjo yakutosha na kwamba walengwa wanapata bila kikwazo. 


PICHANI :Ziara ya Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii, jinsia, wazee na watoto alipotembelea kituo cha afya kaloleni kuona huduma za afya pamoja na kuzungumza na wagonjwa na Wataalam wa Afya katika kituo hicho.

Matangazo

  • NAMNA YA KUPATA KIBALI CHA KUSAFIRI NJE YA NCHI KWA WATUMISHI WA SERIKALI January 16, 2025
  • MATOKEO YA USAILI WA MCHUJO KADA YA MTENDAJI WA MTAA NA KADA YA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU October 06, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 15, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO October 29, 2024
  • Tazama zote

Habari za hivi punde

  • JIJI LA ARUSHA LAZINDUA MITAMBO MIPYA

    January 28, 2025
  • MKURUGENZI KAYOMBO AKABIDHIWA OFISI

    August 21, 2024
  • WANAWAKE NA WASICHANA KUJENGEWA UWEZO WA KISHIRIKI NAFASI ZA UONGOZI

    August 20, 2024
  • NENDENI MKAONGEZE UFANISI

    August 19, 2024
  • Tazama zote

Video

JIUNGE NA MFUMO WA TAUSI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MIRADI ILIYOKAMILIKA
  • MKATABA WA HUDUMA KWA WATEJA
  • SISI NI NANI
  • Urban Sanitation and Hygiene | Mazingira safi Maisha bora

Viunganishi Linganifu

  • TAMISEMI
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Tovuti ya ajira
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Location Map

Wasiliana nasi

    20 Boma Street 23101

    Sanduku la Posta: 3013

    Simu: 0272548072

    Simu ya Mkononi: 0272545768

    Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa