Na Mwandishi Wetu
Serikali imetenga Jumla ya Shilingi Trilioni 2.78 kwaajili ya ujenzi wa miundo mbinu ya Elimu ya Msingi na Sekondari kwa kipindi cha Miaka mitano(5) yaani 2022 hadi 2027 kupitia miradi mbalimbali ya Elimu ikiwemo miradi mikubwa mitatu ambayo ni Mradi wa Kuboresha Elimu Sekondari (SEQUIP), Mradi wa Kuboresha Elimu ya Awali na Msingi (BOOST) na Program ya Kutekekeza Elimu kwa Matokeo (EP4R).
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Innocent Bashungwa wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya Maendeleo ya Elimu nchini kupitia Mkutano na Wanahabari ambao umefanyika leo Septemba 24, 2022 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Mhe. Bashungwa amesema ndani ya mwezi huu fedha zitatolewa kwenye kila Halmashauri ya ujenzi wa Madarasa 8, 000 kwa Maandalizi ya wanafunzi wanaojiunga kidato cha kwanza mwaka 2023.
Waziri Bashungwa ametoa taarifa hiyo ya utekelezaji wa miradi ya Elimu kwa kuwaagiza wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi nchi nzima kusimamia thamani ya fedha hizo katika utekelezaji wa miradi hiyo na kukamilika kwa wakati kama ilvyopangwa na kwa atakayefanya udanganyifu au ubadhilifu wowote wa fedha hizo atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Aidha waziri Bashungwa amesema Kwa mwaka wa fedha 2021/22 kiasi cha Shilingi bilioni 669.85 kimetengwa kwaajili ya utekelezaji wa miundombinu ya elimu Msingi na Sekondari.
Waziri bashungwa ameeleza maeneo kwa upande wa Elimu Msingi yatakayoboreshwa ni pamoja na miundo mbinu ya majengo ya Utawala, ujenzi wa vyumba vya madarasa 9770 na nyumba za walimu 40, ujenzi wa maktaba, matundu ya vyoo, nyumba za walimu, mabweni, mabwalo ya chakula,vyumba vya TEHAMA, na kuboresha Mafunzo kwa walimu na ununuzi wa vifaa vya TEHAMA. Na upande wa Elimu Sekondari ni ujenzi wa Shule mpya za kata 184 Shule 1 kila Halmashauri na Shule 5 za the bweni za wasichana kwa Mikoa ya Katavi, Manyara, Mbeya, Morogoro na Tanga.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Bw. Hargrney Chitukuro amesema kuwa amepokea maelekezo ya Serikali juu ya kusimamia kikamilifu utekelezaji wa miundombinu elimu na Msingi na kwamba atakuwa mstari wa mbele kuhakikisha maelekezo yanaenda sawa kwa ustawi wa wananchi na nchi kwa ujumla.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa