Na Mwandishi wetu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Nchengerwa amewataka Viongozi wa ngazi zote kusimamia utekelezaji wa miradi ya TASAF kwa weledi ambapo jumla ya Miradi 1500 inatarajiwa kutekelezwa katika awamu ya nne ya Mradi wa kupunguza Umasikini Tanzania TASAF kwa mikoa ya Mwanza, Geita, Simiyu, Njombe na Arusha.
Nchengerwa ametoa kauli hiyo alipokuwa akifungua Kikao kazi cha kuzindua utekelezaji wa awamu ya nne ya Mradi wa kupunguza Umaskini Tanzania (TPRP IV), Jijini Arusha ambapo alitoa rai kwa viongozi wa ngazi zote kusimamia miradi hiyo kuhakikisha inatekelezwa kwa thamani halisi.
Mhe. Nchengerwa amsema kiasi cha shilingi Bilioni 130 katika mikoa hiyo mitano itatolewa kwa lengo la kunyanyua kaya masikini hivyo amesisitiza utekelezaji wa miradi ufanyike kwa weledi ili fedha hizo zikatumike kwa makundi ya watu waliokusudiwa.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella amesema Mkoa wa Arusha umepokea kiasi cha shilingi bilion 1.5 kwa kipindi cha mwezi Julai mpaka Oktoba kwa ajili ya kuratibu miradi wa kaya masikini ya TASAF na kuahidi kutekeleza nakusimamia kikamilifu na kwamba hawatomvumulia yeyote atakayefanya vitendo vya ubadhilifu wa fedha hizo.
Kwa upande wake Mbunge wa Arusha Mjini Mhe. Mrisho Gambo amesema uzinduzi wa awamu ya nne kufanyika mkoa wa Arusha ni fursa kwa watu na kaya maskini kwani kutasaidia kupunguza makali na hali duni za maisha ya wananchi.
Jumla ya Halmashauri 33 kutoka Mikoa mitano itanufaika na mradi wa awamu ya nne wa kupunguza umaskini Tanzania TASAF.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa