Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Mhe. Gabriel Daqqarro leo Tarehe 15 Februari 2019 amekabidhi hundi ya mfano yenye thamani ya Sh. Mil 530,000,000/= kwa vikundi 64 vya wanawake na vikundi 36 vya vijana kutoka katika kata 25 za Jiji la Arusha ikiwa ni mikopo ya robo ya tatu kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Akifungua mafunzo ya ujasiriamali kwa vikundi hivyo Mhe. Daqarro amewataka kinamama na vijana kutumia fedha hizo kwa shughuli zilizokusudiwa ili ziweze kuleta manufaa na kuwatoa katika lindi la umasikini.
“Mikopo hii inatolewa ili kuendeleza shughuli za kijasiriamali ambazo ndizo zilizopelekea mkidhi vigezo vya kupata Fedha, Nimatumaini yangu fedha hizi zitawawezesha kuongeza mitaji yenu na kuwapa ari ya kujituma zaidi huku mkizingatia nidhamu ya pesa ili muweze kuzirejesha kwa wakati na makundi mengine waweze kupata fedha hizo” Alisema Mhe. Daqarro
Aliongeza kuwa kwa sasa fedha hizo sio mikopo tena kwa kuwa hakuna marejesho yoyote bali wananchi wameazimwa ili kuweza kujiendeleza kiuchumi hivyo ni wajibu wao kuzirejesha kwa wakati ili wengine waweze kunufaika na fedha hizo.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Jiji la Arusha amesisitiza kuwa kikundi ambacho hakitarejesha fedha zote za mkopo ama kuchelewesha marejesho kwa namna yeyote ile hakitapatiwa mkopo katika mwaka unaofuata ila wale watakaofanya vizuri katika biashara zao na kukuza mitaji wataongezewa kiasi cha kukopa kulingana na hali ya shughuli zao.
Mikopo hiyo inayotolewa kwa mujibu wa Sheria na miongozo inelekeza asilimia kumi ya Mapato ya ndani ya Halmashauri kutolewe kama Mikopo isiyokuwa na riba kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa