Na Mwandishi Wetu
Arusha.
Kila ifikapo April 12 ya kila mwaka Dunia huadhimisha siku ya Kimataifa ya watoto wa mtaani ambapo katika Jiji la Arusha Mstahiki Meya wa Jiji hilo Mhe. Maxmillian Matle Iranqhe alikua Mgeni Rasmi katika tukio maalum la kuadhimisha siku hiyo iliyoandaliwa na Kituo Cha Amani Center kwa lengo kuikumbusha Jamii kuwa jukumu la kuwalea watoto wa mtaani ni la kila mmoja, Tukio ambalo lilitanguliwa na Maandamano ya Watoto wa Mtaani kuanzia katika Mitaa ya Soko Kuu Mjini Kati, Stendi Kuu ya Mabasi ya Mkoa, Mnara wa Uhuru (Makumbusho) hadi katika Uwanja wa Mviringo Kaloleni Jijini Arusha.
Akizungumza Wakati wa Mkutano wa Maadhimisho ya Siku ya watoto wa mtaani mwaka huu Meya wa Jiji la Arusha Mhe Maxmillian Matle Iranqhe pamoja na kuipongeza taasisi ya Amani' Center ametoa Rai kwa Taasisi mbalimbali za kijamii na wadau wa Maendeleo Jijini Arusha na nje ya Jiji hilo kuhamasika kuungana na jitihada za wazi zinazofanywa na Jiji hilo pamoja taasisi kama Kituo Cha Amani Center amesema Jiji la Arusha imeafanikiwa kutenga eneo la hekari tano (5) katika Kata ya Olmoti kwa ajili ya kuwajengea makazi watoto wa mtaani ikiwa ni pamoja na kuwafungulia Shule ya ufundi katika eneo hilo.
Meya amesema lengo la jitihada hizo ni kukabiliana na wimbi la ongezeko la watoto wa mtaani Jijini humo na kuliokoa Taifa dhidi ya makundi hatari ya majambazi, wezi, vibaka, watumiaji wa madawa ya kulevya na athari zingine mbalimbali kwani kwa mazingira wanayokulia ni rahisi zaidi kuishia kwenye makundi ya aina hiyo hali inayopelekea kutokua na nguvu kazi ya Taifa ikizingatiwa kua Vijana ni Taifa la Sasa na baadaye.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa