Vijana na wanawake wametakiwa kuunda vikundi kwa kufuata taratibu ili waweze kupatiwa mikopo ya asilimia 10.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Thomas Sabaya alipokuwa akizungumza na viongozi wa kata na mitaa pamoja na wataalamu wa Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Amesema mikopo hiyo ipo kwa ajili ya vijana na wanawake hivyo wachangamkie fursa zakuwaleta maendeleo na waache kulalamika.
" Huu sio wakati wakulalamika, undeni vikundi kwa kufuata taratibu kisha ombeni mikopo ya 10% mfanye biashara zakuwaingizia vipato",alisema.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa yupo katika ziara ya siku 10 katika Wilaya ya Arusha ambapo atapita kata kwa kata kuzungumza na viongozi wa chama na kutatua kero za wananchi.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa