Mkuu wa Wilaya ya Arusha Felician Mtahengerwa amewataka watendaji wa Kataka Wilaya hiyo kujiridhisha na uraia wa wananchi wanahitaji vitambulisho vya Taifa.
Kauli hiyo ameitoa alipokuwa akigawa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi katika kata ya Levolosi, Jijini Arusha.
Amesema kitambulisho cha Taifa ni muhimu kwa kila mwananchi kwani ni utambulisho wa kila Mtanzania hivyo visitumike hadi kwa ambao sio watanzania.
Pia, amewataka wananchi kutoruhusu vitambulisho vyao vitumiwe na watu wengine kwani inaweza kumpelekea mtu kuingia kwenye matatizo ya kisheria.
Amesisitiza kuwa wananchi wote ambao hawajachukua vitambulisho vyao kwenye ofisi zao za kata wakachukue maana kwanzia sasa namba za NIDA hazitatumika kwenye maeneo mengi bali ni Kitambulisho chenyewe.
Katika Wilaya ya Arusha Jumla ya Vitambulisho 338,325 vimeshatolewa na vitambulisho 148,864 vitatolewa kwa awamu hii ya pili katika ofisi za Kata.
Nae, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Arusha ameitaka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA Mkoa wa Arusha kumalizia utoaji wa Vitambulisho vilivyobaki.
Kwa upande wake, Afisa Usajili kutoka NIDA Julieth Raymond amesema hadi sasa Vitambulisho vilivyotolewa ni asiliamia 93 kwa Wilaya ya Arusha.
Amesisitiza kuwa juhudi zinaendekea kuhakikisha asilimia 7 zilizobaki zinamaliziwa na kila mwananchi anaestahili kupata kitambulisho anapata.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa