Ujenzi upo katika hatua za umaliziaji. Hadi kufikia mwishoni mwa mwezi huu mradi utakuwa umekamilika na barabara itaanza kutumiwa rasmi na wananchi.
Ujenzi wa barabara ya Sombetini – Ffu wenye kipande chenye urefu wa kilometa 2.1 unatekelewa na kampuni ya Sinohydro Co-Operation Ltd ya nchini China chini ya mradi wa uboreshaji miji na majiji nchini (TSP) awamu ya tatu una gharama ya sh. Bilioni 22. 3
Mradi huo unajumuisha pia ujenzi wa barabara za Oljoro-Murriet km 3, Njiro km 2.72, Soko la Krokon km 0.75, Ngarenaro km 4.3 , uwanja wa michezo katika shule ya msingi Ngarenaro na bwawa la kuhifadhia taka ngumu katika dampo la Murriet.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa