Tarehe 18 Agosti 2019 Umoja wa vijana Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Arusha ukiongozwa na Katibu wa vijana Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya Ndg.Ibrahimu Kijanga ambaye ameongozana na Katibu Hamasa na chipukizi wilaya Ndg.Abdi Mutu Marijani, Mjumbe wa kamati ya utekelezaji UVCCM mkoa Ndg.John Nkini na viongozi wengine wa CCM wamejumuika kuchangia damu katika kituo cha afya Levolosi jijini Arusha.
Hii ikiwa ni kampeni ya kuchangia damu kufuatia ajali ya moto iliyotokea mkoa wa Morogoro iliyosababisha mlipuko wa tanki la mafuta mnamo tarehe 10 Agosti 2019 na kupelekea vifo vya watu wengi na majeruhi.
Katika kampeni hiyo ya kuchangia damu Ibrahimu Kijanga amehamasisha vijana kujitokeza kwa wingi ili kuokoa maisha ya watanzania kwa kuchangia damu kwani uhitaji wa damu salama ni mkubwa kuliko akiba iliyopo katika benki ya damu salama.
“Lakini nitoe wito tuendelee kushiriki katika zoezi la kuchangia damu kuokoa maisha ya wenzetu kama ilivyo desturi yetu ili kusaidi pale panapotokea majanga kwani tukiendelea kufanya hivi tunajenga upendo, mshikamano na umoja kama mnavyotambua Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli anatuhimiza tushiriki kuokoa maisha ya wenzetu wanapopata majanga” alisema Ibrahimu Kijanga.
Pichani: Mjumbe wa kamati ya utekelezaji UVCCM mkoa Ndg.John Nkini akichangia damu salama katika kituo cha Afya Levolosi
Kauli mbiu: “Changia damu okoa maisha"
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa