Leo tarehe 17/09/2019 timu ya madaktari kwa kushirikiana na Mganga Mkuu wa Jiji la Arusha Dkt. Simon Chacha wamezindua huduma ya upasuaji kwa mama wajawazito katika kituo cha afya Daraja Mbili kilichopo Jiji la Arusha.
Akiongoza zoezi hilo Mganga Mkuu wa Jiji la Arusha Dkt. Simon Chacha amesema kuwa kuzinduliwa kwa huduma hiyo kutawapunguzia wananchi gharama kwa kuwa huduma hiyo ni bure katika vituo vya afya vya serikali ukilingalinganisha na vituo vingine.
Dkt. Chacha ameongeza kuwa licha ya kupunguza gharama kwa wananchi lakini pia kutolewa kwa huduma hiyo kutasaidia kupunguza msongamano kwa mama wajawazito kujifungulia katika hospitali za mjini kama vile hospitali ya rufaa ya Mount Meru.
“Kwa sasa hivi huduma ya upasuaji kwa mama wajawazito inapatikana katika vituo vya afya vitatu vya Jiji la Arusha ambavyo ni Kaloleni, Levolosi na Daraja Mbili na kituo kinachofuata kuzinduliwa huduma hii ni Murriet” alisema Dkt. Chacha
Timu ya madaktari wa kituo cha afya Daraja mbili katika picha ya pamoja na Mganga Mkuu wa Jiji la Arusha Dkt. Simon Chacha (wa tatu kutoka kulia) baada ya kukamilisha upasuaji wa kwanza
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa