Halmashauri ya Jiji la Arusha leo Tarehe 25/04/2019 imezindua jukwaa la wasanii wa Jiji la Arusha lililofanyika katika uwanja wa Jiji uliopo jirani na mzunguko wa kuelekea kijenge Jijini Arusha
Jukwaa hilo limehusisha wasanii wa fani zote wakiwemo waimbaji, ngoma za asili, wachekeshaji, wapishi wa vyakula vya kitamaduni pamoja na mafundi wa fani mbalimbali.
Kila msanii alipata fursa ya kuonyesha uwezo wake wa kisanaa kwa lengo la kujitangaza na kukuza soko la kazi ya sanaa kupitia wadau wa maendeleo.
Sambamba na maonyesho ya vipaji pia wasanii walipata fursa ya kupatiwa elimu juu ya umuhimu wa wasanii kushiriki shughuli za uchaguzi wa serikali za mitaa kwa amani, faida za utunzaji wa vyanzo vya maji na mazingira, faida ya usajili wa BASATA na COSOTA kwa msanii, utamaduni wa kiutalii na umuhimu wa wasanii kushiriki katika matukio ya kitaifa hususan mkesha wa mwenge.
Jukwaa la wasanii Jiji la Arusha limezinduliwa na katibu Tawala wa wilaya ya Arusha Mjini Ndg, David Mwakiposa na katika hotuba yake aliwaasa wasanii kutangaza shughuli za maendeleo zinazofanywa na serikali kwani sanaa ni muhimili mkubwa katika kufikisha ujumbe kwa jamii, kuelimisha na kuburudisha.
Jukwaa la wasanii Jiji la Arusha linatarajiwa kufanyika kila mwaka lengo ikiwa ni kuthamini na kutambua vipaji vilivyopo katika jamii katika kuleta maendeleo kwa taifa letu na kukuza pato la taifa kupitia sanaa.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa