Shirika la The Global Alliance for improved Nutrition (GAIN) limetoa mafunzo maalumu kwa Menejimenti ya Halmashauri ya Jiji la Arusha kuhusu namna vijana watakavyo shiriki katika mifumo ya chakula.
Bwana, Sadam amesema lengo la mpango huo wakuwashirikisha vijana ni kuwajengea uwezo na kutumia fursa zilizopo kwenye mifumo ya chakula.
Pia, amesisitiza kuwa mradi huo utawasaidia vijana pia kujua namna yakutumia lishe bora itakayo wasaidia kujenga afya zao bora na jamii kwa ujumla.
Akizungumza katika mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Mhandisi Juma Hamsini ameshauri shirika hilo la GAIN pia kulinda vyanzo vya Maji.
Juma Hamsini amewashauri pia, Elimu ya mifumo ya chakula pia iende kwa wananchi wengine ili waweze kupata uelewa mpana.
Shirika la GAIN, limepanga kuanzisha mfumo wa chakula utakao washirikisha vijana katika kilimo na uzalishaji wa chakula bora kwa ujumla na mafunzo hayo yataendelea kutolewa kwa Wahe.Madiwani na watendaji wa kata.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa