Viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) kata ya levolosi jijini Arusha wamempongeza mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dr. Maulid Suleiman Madeni kwa kuanzisha operesheni ya ukusanyaji wa mapato yenye lengo maalum la kuongeza mapato ya jiji.
Pongezi hizo zimetolewa wakati viongozi hao walipomtembelea Mkurugenzi wa jiji ofisini kwake mapema leo hii ambapo Miongoni mwa changamoto zilizoainishwa na katibu wa ccm kata ya levolosi bi. Aisha mara ni Pamoja na mpangilio mbovu wa stendi ndogo ya Kilombero na stendi ndogo ya Miami hali inayopelekea changamoto ya msongamano wa watu kwani hakuna mpangilio mzuri wa ruti za daladala wakati wa kupakia abiria
Changamoto nyingine inayoikabili kata ya levolosi ni mazingira kuwa machafu kutokana na wimbi kubwa la wafanyabishwara wadogo almaarufu kama machinga kutozingatia usafi wa mji.
Kwa upande wa elimu kata ya levolosi ina ukosefu wa Shule ya Sekondari, hivyo wamemuomba Mkurugenzi kama ndani ya shule ya Msingi Levolosi kuna eneo kubwa ambalo kuna uwezekano wa kujenga Shule ya Sekondari kwa kiwango Cha ghorofa, wataalamu wa halmashauri watembelee eneo husika na kufanya upembuzi yakinifu.
“Wafanyabiashara wote Wajenge tabia ya kulipa kodi kwa wakati iIi Kuepuka usumbufu kwa Serikali na waache tabia ya kulipa kodi kwa njia ya zisizo sahihi, tunawaomba wafuate utaratibu uliowekwa na serikali au Halmashauri” alisema Bi. Aisha wakati akisoma taarifa yake kwa Mkurugenzi wa Jiji
Aidha aliongeza kwa kusema kuwa Miundo mbinu katika Soko la Kirombero iboreshwe hasa kwa upande wa mfumo wa maji taka na Ukuta wa soko la vitunguu Kilombero ujengwe kwa kuongezwa urefu kwa ajili ya usalama wa bidhaa hiyo .
Naye dr. madeni aliwashukuru viongozi hao wa ccm kata ya levolosi kwa kumtembelea na kuahidi kuzifanyi akazi changamoto zote walizoziainisha.
“kitu kimoja tu ninachowaomba viongozi wenzangu, isiwe tu kuunga mkono operesheni ya mapato kwa mameno bali ningependa operesheni zijazo tuambatane bega kwa bega hadi kwa wananchi kuhamasisha ulipaji wa kodi na ushuru kwani mapato haya ndio mhimili mkuu wa Halmashauri yetu na Taifa kwa ujumla ” Alisema Dr. Madeni
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa