Wakuu wa Idara na Vitengo Halmashauri ya Jiji la Arusha wapatiwa mafunzo ya mpango mkakati miaka mitano ijayo.
Na Mwandishi wetu .
WAKUU wa Idara na wakuu wa vitengo katika Halmashauri ya Jiji la Arusha wametakiwa kuandaa mpango Mkakati wa kipindi cha miaka (5) mitano ijayo katika kila idara ikiwa ni kuwezesha utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika Halmashauri hiyo ikiwa ni pamoja na kuhudumia wananchi wa Jiji la Arusha .
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Rebecca Mongi akizungumza na watumishi hao katika ukumbi wa mikutano wa Shule ya Arusha Jijini Arusha alisema kuwa mpango Mkakati huo utakuwa ni matokeo ya mafanikio na maendeleo katika taasisi hiyo kwa kipindi cha miaka (5) mitano ijayo.
Bi Mongi anasema kuwa mpango kazi bora utawezesha miradi ya maendeleo kutekelezwa kwa mujibu wa taratibu na sheria zilizopo na kudai kuwa uongozi wa Halmashauri utaendelea kutoa fursa za mafunzo kwa watendaji ili kuwawezesha kuandaa mpango bora kwa faida ya jamii wanayoihudumia
‘’Nimefurahi kuwa mumeonyesha ukomavu wa hali ya juu kwa kukubali kuhudhuria mafunzo haya bila kuwa na kisingizio na udhulu wakutoshiriki ,naamini mpango ambao mtaandaa utakuwa wa viwango vya juu’’ alisema Mongi.
Kwa upande wake Mwezeshaji wa mafunzo hayo Abdallah Mvungi ambaye ni Afisa Uwekezaji Jiji la Arusha ,alisema kuwa taasisi yenye mpango mkakati bora na sahihi utaweza kufanikiwa na kuwaletea wananchi wake maendeleo .
Bw,Mvungi alisema kuwa mafunzo ya mpango mkakati wa Halmashauri ya Jiji la Arusha utaleta tafsiri sahihi ya mafanikio kwa wananchi wa Jiji la Arusha kwa kutekeleza miradi ambayo ni kero na nikwazo kwa maendeleo ya jamii .
Naye Kaimu Mchumi wa Jiji la Arusha Mathias Shindika akizungumzia mafunzo hayo alisema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa watendaji wakuu wa Halmashauri lengo ikiwa ni kuwawezesha na kuwakumbusha namna bora ya kuandaa mpango mkakati.
Shindika alisema kuwa mafunzo waliyopata yamewafungua na kwamba wanatarajia kuona matokeo chanya ambayo watayaona wakati wakuandaa mpango kwa kila idara .
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa