Bodi za shule zote katika Halmashauri ya Jiji la Arusha zimetakiwa kuhakikisha zinaondoa wafanyabiashara wa vitu mbalimbali katika maeneo ya shule ili kuwafanya wanafunzi wale chakula cha shule.
Kauli hiyo, imetolewa na Kaimu mwenyekiti wa kikao cha lishe robo ya tatu Daktari Nindwa Maduhu alipokiwa akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti ambae pia ndie Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Amesema, utoaji wa chakula katika shule ni muhimu kwa kumjengea mwanafunzi mazingira rafiki ya kusoma.
Aidha, ametoa wito kwa wazazi kuchangia chakula kwa watoto wao pindi wanapokuwa shuleni kwani wapo baadhi yao hawachangii na hivyo kusababisha watoto wao kukosa chakula.
Pia, ametaka elimu ya lishe itolewe kwa wazazi wenye watoto wa umri chini ya miaka 2 ili kupunguza udumavu kwa watoto hao.
Kikao cha lishe robo ya tatu kimefanyika kwa kupitisha maazimio mbalimbali ikiwemo kuendelea kutoa elimu kwa wazazi kuhusu uchangiaji wa chakula katika shule.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa