Wananchi wa Jiji la Arusha wapongeza Serikali kwa kuanza ujenzi wa Jengo la Utawala la Halmashauri
Na Mwandishi Wetu
WANANCHI walioshiriki Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Arusha la robo ya tatu wamepongeza Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suhulu Hassan kwa kutoa fedha kuanza ujenzi wa Jengo la Utawala la Halmashauri ya Jiji la Arusha kwamba Jengo lilopo kwa sasa halina hadhi ya Jiji.
Neema Laizer Mkazi wa Ungalimited akizungumza mara baaada kumalizika mkutano wa Baraza hilo uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha alisema kuwa kujengwa kwa jengo hilo kutaleta hadhi ya Jiji kwa kuzingatia kuwa Halmashauri ya Jiji la Arusha iko katikakati ya mji wa Arusha.
Bi Laizer alisema kuwa Arusha ni mji wa Kitalii na hivyo unapaswa kuwa na hadhi kwa kupambwa na miundo mbinu bora ya barabara na majengo ya kisasa.
Meya wa Jiji la Arusha Maximilian Iranqhe akielezea Jengo hilo alisema kuwa Baraza la madiwani la limepitisha ujenzi wa Jengo hilo na kwamba madiwani wa Halmashauri yao nia yao ni kuona Jiji la Arusha linaendelea kuwa namba moja.
"Niseme kuwa Jengo hili linajengwa katika eneo hili la Parking ya Halmashauri na kwakweli tunampongeza Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali yake kwa kutupatia upendeleo huo ,nawahakikishia wananchi wa Jiji la Arusha kuwa Kazi inaendelea na Mimi na Baraza langu la Madiwani tutahakikisha kuwa ujenzi huu unakamilika kwa wakati ."alisema Meya
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dk.John Pima alisema kuwa tayari Halmashauri hiyo imepokea kiasi cha Tshs milion 750 kutoka Serikali kuu kwa ajili ya kuanza msingi wa Jengo hilo na kuwa Halmashauri ya Jiji la Arusha katika awamu hiyo ya msingi itatoa milion 160 ikiwa ni fedha zinazotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo.
Dk.Pima alisema kuwa ujezi huo umeanza kwa maandalizi na kwamba nia ya Uongozi wa Halmashauri hiyo nikuona ujenzi huo unakamilika kwa wakati.
Kimsingi alisema kwa sasa watumishi wa Halmashauri hiyo wanapata adha ya ofisi na kwamba ofisi zao ziko katika maeneo mbali mbali kama vile Njiro, Depot Kilombero na kuwa baada yakukamilika kwa ujezi wa jengo hilo watumishi watakaa pamoja .
Dk.Pima alisema kuwa Jengo hilo linatarajia la gorofa sita na litaweza kukidhi mahitaji ya ofisi za watumishi zinazohitajika.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa