Na Mwandishi wetu
Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela amewataka wananchi wa Mkoa wa Arusha kuwa makini na mikataba wanayoingia kwa ajili ya biashara au shughuli yeyote kwa kuhakikisha wanaisoma kabla ya kusaini.
Mhe. Mongela ametoa kauli hiyo wakati a kuzungumza na wananchi katika Kata ya Murieti kuhusu kero zao ambapo alibaini kuwa baadhi ya wananchi wamesaini mikataba bila kusoma na imewaumiza.
Anasema kuwa ni vyema wananchi wakaomba kusomewa na kufafanuliwa mikataba kabla yakusaini kwa kuwa baadhi ya mikataba imeandaliwa kwa makusudi kuumiza watu na kuwa walengwa wanatakiwa na ufahamu wa mikataba husika.
Katika hatua nyingine amezitaka taasisi za Serikali kutatua kero za wananchi kwa kuwapatia huduma kwa wakati ikiwa ni huduma ya maji na umeme.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa