Msimamizi wa uchaguzi Jimbo Dkt. John Pima amewataka wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Jimbo, Kata, maofisa uchaguzi na afisa ugavi wa Halmashauri kufuata taratibu za uchaguzi zilizotolewa na tume ya uchaguzi ili kujenga mazingira rafiki kwa wapiga kura na kupelekea uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 28, 2020 kuwa huru na haki.
Dkt. Pima ametoa maelekezo hayo alipokuwa akifungua mafunzo kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Jimbo, Kata, maofisa uchaguzi na afisa ugavi wa Halmashauri mapema leo tarehe 7 Agosti 2020 katika ukumbi wa mikutano Ofisi yaMkuu wa Mkoa wa Arusha.
Dkt. Pima amesisitiza kuwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzingazi ya Jimbo, Kata, maofisa uchaguzi na afisa ugavi wa Halmashauri wanatakiwa kufahamu kuwa wameaminiwa na kuteuliwa kwa sababu wana uwezo wa kufanya kazi hiyo hivyo mambo muhimu wanayotakiwa kuzingatia ni kujiamini na kujitambua nakwamba wanapaswa kuzingatia katiba ya Nchi, Sheria za uchaguzi na kanuni zake, maadili ya uchaguzi na maelekezo yote yaliyotolewa na tume.
Mafunzo yatafanyika kwa siku 3 kuanzia tarehe 7-9 Agosti,2020 kwa lengo la kubadilishana uzoefu, kujadili namna ya kufanikisha zoezi la Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 pamoja na kuelekezana namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza katika hatua zote za uchaguzi.
***********************************************************************************************************
Picha: Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Jimbo, Kata, maofisa uchaguzi na afisa ugavi wa Halmashauri wakipatiwa mafunzo ya uchaguzi.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa