Watendaji kata na Wataalam wa Afya watakiwa kusaidia huduma ya afya
Na Mwandishi wetu
Watendaji kata katika Halmashauri ya Jiji la Arusha watakiwa kushirikiana na wataalm wa afya katika kuhakikisha wananchi wa kata zao wanapata huduma stahiki pamoja na kuendelea kuwa wawajibikaji kwa kufanya kazi zao kwa uadilifu na kufuata dhana ya ushirikishwaji hatimaye kutoa huduma ya Afya yenye ufanisi.
Akizungumza na Watendaji kata wakati akizindua kampeni ya Nisaidie niishi mimi na mama yangu Kaimu Mkurugenzi Bi. Namnyaki Laitetei alisema kuwa huduma ya afya inahitaji ushirikiano baina ya watendaji na wataalamu wa afya kwa kuwa afya bora ni msingi wa maendeleo ya jamii yeyote Duniani.
Bi. Laitetei alisema kuwa huduma bora ya afya ni matokeo ya maendeleo katika jamii yeyote na kwamba huduma bora itafikiwa kwa ushirikiano wa wadau wa afya watendaji wa kata wakiwa ni miongoni mwao.
“Mnapaswa mfanye kazi zenu kwa kutekeleza na kufuata misingi ya Utawala bora kwa kufanya ushirikishwaji wa wadau mbalimbali ili kuendelea kutoa huduma zenye ufanisi” alisema Laitetei
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Dk. Kheri Kagya alisema kuwa huduma za afya katika Jiji la Arusha zinafanywa kwa weledi mkubwa na kuwataka kuendelea kusaidia upatikanaji wa huduma hiyo kwa wananchi ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Mh.Rais Dk.John Pombe Magufuli kwa kuhudumia wananchi kwa moyo bila kuchoka .
‘’Hatutaki na hatuwezi kukubali kile wanachotuletea Serikali kipotee, ni muhimu sote tuendelee kuwa wasimamizi wazuri wa vitendea kazi na vifaa tiba ili vitumike kwa malengo yaliyokusudiwa” alisema Dk.Kagya.
Dk.Kagya alisema matarajio ya serikali nikuona wananchi wanapata huduma bora na katika kufikia mafanikio hayo kila mtu hususani wataalm wa afya na watendaji wa kata wanajukumu lakusaidia kufikia nia njema.
Halmashauri ya Jiji la Arusha ni miongoni mwa Halmashauri zinazofanya vizuri katika huduma ya afya hapa nchini.
Picha za matukio kikao cha Wataalm wa Afya na Watendaji wa Kata wakati wa kikao cha kujadili maendeleo ya afya na mtoto.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa