Maadhimisho ya siku ya walemavu duniani yamefanyika mapema leo Tarehe 3/12/2019 katika ukumbi ya shule ya msingi ya Arusha mgeni wa heshima akiwa ni Mhe. Gabriel Daqarro akiambatana na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt Maulid S. Madeni, Mganga mkuu wa Jiji Simon Chacha na viongozi wa kamati ya watu wenye ulemavu wilaya ya Arusha. Katika maadhimisho hayo kauli mbiu ikiwa ni “Ufikikikaji kwa maisha yajayo utakua bora zaidi”.
Akisoma risala kwa mgeni wa heshima kwa niaba ya watu wenyeulemavu Ndg. Anziran Saidi amesema wanaishukuru Halmashauri ya Jiji kwa kutenga asilimia 2 ya mapato kwaajili ya kutoa mikopo kwa vikundi vya watu wenye ulemavu ambapo vikundi 23 vimepata mikopo yakiasi cha milioni 100, pamoja na Halmashauri kugharamia watu wawili wenye ulemavu kushiriki maadhimisho ya siku ya walemavu katika ngazi ya Taifa .
Katika maadhimisho hayo watu 15 wenye ulemavu wa viungo wamegawiwa viti mwendo, mafuta kwaajili ya walemavu wa ngozi, miwani ya kupunguza mwanga wa jua pamoja na kofia kwaajili ya kukinga na mionzi ya jua .
Hata hivyo watu wenye ulemavu wameainisha changamoto wanazokumbana nazo kuwa ni ukosefu wa ofisi za kufanyia shughuli zao, muamko mdogo wa fursa ya mikopo, marejesho ya vikundi vya watu wenye ulemavu kusuasua, upungufu wa vifaa visaidizi kama viti mwendo, fimbo nyeupe, mafuta ya albino, magongo pamoja na uchache wa wakalimani wa lugha ya alama kwa viziwi.
Akizungumza katika hafla hiyo Mhe.Daqarro amesema katika Jiji la Arusha takwimu zinaonyesha kuwa wapo watu wenye ulemavu 627 kati ya hao wanawake ni 305 na wanaume ni 322 ambapo wenye ulemavu wa wa viungo ni 342, wenye ulemavu wa ngozi ni 52, wenye ulemavu wa kusikia ni 53, wenye ulemavu wa akili ni 128 na wenye ulemavu wa uti wa mgongo ni 5.
Pia ameongeza kua katika Jiji la Arusha jumla ya watu 46 wenye ulemavu wamepatiwa mikopo isiyokua na riba yenye thamani ya Millioni 9.2 lakini pia watu wemye ulemavu 74 kutoka katika kata zote za wilaya ya Arusha walipatiwa viti mwendo 74 pamoja na pikipiki 2 za matairi matatu yenye thamani ya Millioni 7.6 pamoja na watu 360 wamegawiwa kadi za bima ya afya bure.
Mhe. Gabriel Daqarro amehitimisha maadhimisho hayo kwa kuwasihi Maafisa ustawi wa jamii na Mkuu wa kitengo hicho kuwapa kipaumbele watu wenye ulemavu kuliko watu wengine hivyo kwa kila robo ya mwaka kati ya vikundi vitakavyo peleka maombi au kusajiliwa kwaajili ya kupatiwa mkopo kundi la walemavu visipungue vikundi vitano vitakavyo patiwa mkopo.
Mwisho.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa