Mkuu wa mkoa wa Arusha ambae pia ni kiongozi mkuu wa shughuli za kiserikali ngazi ya mkoa Mh. Mrisho Gambo amehutubia maelfu ya wafanyakazi katika mahadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani Mei Mosi-2018. Ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni "kuunganishwa kwa Mifuko ya hifadhi za jamii kulenge kuboresha mafao ya mfanyakazi".
Mkuu wa mkoa alikagua maandamano mbalimbali ya wafanyakazi. Ambapo maandamano hayo yalianzia katika Ofisi za Halmashauri ya Jiji la Arusha. Pamoja na hayo pia alitoa zawadi mbalimbali kwa wafanyakazi bora. Ameyafanya hayo ili kuchochea hari ya wafanyakazi katika kufanya kazi.
Mfanyakazi bora Halmashauri ya Jiji la Arusha Ndg. Frank Sanga ambaye ni Afisa Tawala akipokea cheti kutoka kwa Mgeni rasmi Mh. Mkuu wa mkoa wa Arusha katika sherehe za mahadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani yaliyofanyika katika viwaja vya Sheikh Amri Abeid Mkoani Arusha.
Jiji la Arusha liliibuka washindi wa kwanza katika maandamano ya miguu chama cha TALGWU, Ambapo mgeni rasmi aliwazawadia kombe. Alikadhalika watumishi mbalimbali wa jiji la Arusha walipata tuzo ya wafanyakazi bora.
Mkuu wa mkoa wa Arusha pia alisikiliza kero mbalimbali zinazowakumba wafanyakazi ikiwa ni pamoja na mishahara duni. Ambapo amesema alisema kero amezisikia na atazifikisha kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mkuu wa mkoa alimalizia kwa kusema anawapongeza wafanyakazi na wananchi wa jiji la Arusha kwa kuendelea kuitunza amani ya Tanzania ambapo kwa miaka michache iliopita ilionekana kusuasua.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa