Katika kuelekea mitihani ya kidato cha Nne Afisa Elimu Sekondari Jiji la Arusha Bw. Valentine Makuka amewaasa wazazi na walezi kutoa ushirikiano kwa walimu ili kuinua ufaulu kwa wananfunzi
Bw. Makuka ambaye ndie alikuwa mgeni rasmi mahafali ya kidato cha nne katika shule ya sekondari Moshono iliyopo Jijini Arusha ametoa rai hiyo wakati alipokuwa akizungumza na wazazi, wanafunzi pamoja na waalimu wa shule hiyo wakati wa mahafali hayo yaliyofanyika hapo jana Tarehe 19 October 2018.
Bw. Makuka amesema kuwa kuna baadhi ya wazazi na walezi hawatoi ushirikiano wa kutosha kwa walimu katika kufatilia mienendo ya wananfunzi matokeo yake wanawaachia walimu peke yao katika kusimamia malezi ya watoto jambo ambalo limekuwa likichangia kwa asilimia kubwa wanafunzi kufeli kwani wanakosa unagalizi wa pande zote mbili.
“ Napenda kutoa pongezi kwa wanafunzi wote mnaotarajia kufanya mitihani yenu ya kidato cha nne kwa hatua kubwa na nzuri mliyofikia kwani wapo baadhi ya wanafunzi walioshindwa kuendelea na masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo mimba, makundi mabaya ya mitaani, magonjwa na hata vifo, mzingatie mliyoelekezwa na walimu wenu na hatimaye muweze kufaulu vizuri na kuiletea sifa nzuri shule yetu”. Alisema bw. Makuka
“kwa walimu wote watakaochangia wanafunzi kupata alama ya F katika masomo yao kwa asilimia zaidi ya 50 katika mitihani, naomba msahau na mjifute katika mikakati ya kupanda vyeo, huo ndio mpango mkakati wa kuhakikisha wanafunzi wanafaulu na sisi walimu tunawajibika” aliongeza Afisa Elimu huyo
Pia ameongeza kwa kusema kuwa walimu kwa kushirikiana na vyombo vya habari kuna mkakati wa kuazisha kampeni maalumu ya kuongeza uwezo wa matumizi ya lugha ya kingereza kwa kuendesha midahalo kwa wanafunzi wa shule zote za serikali zilizopo Jiji Arusha.
Sherehe za mahafali ya kidato cha nne hufanyika kila mwaka katika viwanja vya shule hiyo ya Moshono na kwa mwaka huu wa 2018 idadi ya wahitimu ni wanafunzi 75.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa