Na Mwandishi Wetu
Arusha.
Wazee Jijini Arusha wameiomba Serikali kutunga sheria ya kusimamia wazee ili kuondosha ukatili dhidi yao
Rai hiyo imetolewa na Kassim Selamkwa Katibu wa Wazee Wilaya ya Arusha wakati walipo kutana jijini Arusha katika Maadhimisho ya Siku ya kupinga ukatili wa Wazee yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Jiji la hilo.
Amesema, vitendo vya kikatili kwa makundi maalumu hasa kwa wazee vinaendelea kufanyika nchini licha ya kuwa vitendo hivyo bado vinaendelea kukemewa.
Aidha ameongeza imani za kishirikina zinachochea ukatili kwa wazee na kutoa wito kwa viongozi wa dini na kisiasa kuelimisha jamii juu ya haki za wazee na kuachana na ramli chonganishi.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Maximilian iraqhe amewataka wazee kukemea vitendo vya ukiukwaji wa maadili ndani ya jamii ikiwemo ushoga na kuwataka wazee hao kuacha kuwaendekeza watoto wao kwa kuwapatia mali badala yake watoto watafute mali zao wenyewe ili kuepusha migogoro baina ya wazazi na watoto.
Sambamba na hayo inaelezwa kuwa idadi ya wazee waliopo katika Jiji la Arusha ni 9, 307 wanaotambulika mpaka sasa.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa