Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameongoza zoezi la kuwakabidhi mikopo isiyokuwa na riba akina Mama 600 wa jiji la Arusha ikiwa ni marejesho ya fedha za madereva Pikipiki 200 walizokabidhiwa kama mkopo wa kuwawezesha kujikwamua kiuchumi na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi Waziri Mhagama amesema kuwa akina mama hao wanatakiwa kutumia fedha hizo katika makusudio ya kufanya biashara nakuahidi Ofisi yake kuendelea kutoa ushirikiano.
Nae Mkuu wa mkoa wa Arusha mhe. Mrisho Gambo amesema ameamua kuwakopesha akina mama kwa kuwa wamekuwa wakihitaji mtaji mdogo ili kutengeneza mazingira ya kufanya biashara zitakazowasaidia kuinua kipato chao binafsi na Taifa kwa ujumla
“Fedha hizo mlizokabidhiwa leo sio za msaada bali ni za mkopo hivyo mnapaswa kuwa waaminifu na kurejesha kwa wakati ili ziweze kuwasaidia wengine” alisema mkurugenzi wa jiji la Arusha Ndg. Athuman Kihamia wakati wa ufunguzi wa ghafla hiyo.
MWISHO.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa