Jumla ya wenyeviti 154 wameapishwa mapema leo Tarehe 26 Novemba 2019 katika ukumbi wa shule ya Sekondari Arusha na Hakimu wa Mahakama ya mwanzo Mhe. Goodluck Mbowe.
Akizungumza katika hafla hiyo msimamizi wa uchaguzi Wilaya ya Arusha Ndg.Msena Bina amewapongeza wenyeviti hao na kuwasihi kusimamia haki na sheria, kufanya kazi kwa uaminifu kwani ndio walioonekana wanafaa kwenda na kasi ya Mh Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Hata hivyo hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kisiasa ambao ni Katibu wa CCM Wilaya Ndg. Denis Mwita Zakaria, Mwenyekiti wa madiwani CCM Mhe. Tojo, Ndg. Elirehema Nko katibu wa Madiwani CCM pamoja na Ndg. Issa Said Omary mjumbe wa kamati ya madiwani CCM.
Ndg.Denis Mwita ambaye ni katibu wa CCM Wilaya amewaahidi wenyeviti hao kupewa ushirikiano na kamati ya siasa ya Wilaya na kujenga mahusiano mazuri na watendaji wa serikali za Mitaa kwani katika Mitaa mingi maendeleo yanakwama kwa sababu ya mahusiano mabaya baina ya viongozi wa Mitaa husika na baada ya kuapishwa wanastahili kupewa mafuzo ambapo msimamizi wa uchaguzi wilaya Ndg. Msena amewaambia mafuzo watapata katika chuo cha Hombolo cha Serikal za Mitaa .
Aidha Ndg.Msena Bina amewaainishia wenyeviti majukumu yao ikiwa ni pamoja na kuwa wenyeviti wa mikutano yote ya mtaa, Kusuluhisha migogoro midogomidogo ambayo haistahili kuitishwa mikutano ya kamati za mitaa au kupelekwa kwenye baraza la kata, kuwa wasemaji wa Mitaa, kuhimiza wakazi wa Mitaa kushiriki kwenye shughuli za maendeleo na sherehe za kitaifa pamoja na mikutano ya hadhara itakayo andaliwa katika mtaa, halmashauri ya Jiji au Serikali kwa ujumla.
Kuwa wawakilishi wamitaa kwenye kamati ya maendeleo ya kata, Kutekeleza kazi watakazopewa na kamati ya Mtaa, mkutano wa mtaa pamoja na kamati ya maendeleo ya Kata yaani yale maadhimio yanayotokanana katika vikao vyote vya kata. Kusimamia utekelezaji wa kazi na majukumu ya kamati ya Mtaa, kusimamia utunzaji wa Rejesta za wakazi wote wa mtaa na kuwafahamu wakazi wa Mitaa yao bila kubagua dini, kabila, chama au rangi ilimradi ni mtanzania na kwa yule asiye mtanzania apelekwe kwenye vyombo vya usalama.
Mwisho.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa