Halmashauri ya jiji la Arusha kwa kushirikiana na Lions Club Arusha Arusha imetoa huduma ya uchunguzi na matibabu ya macho bila malipo kwa zaidi ya wakazi 776 wa Kata ya Murriet na Terrat Jijini Arusha.
Huduma hiyo imetolewa Tarehe 2-3 mwezi Februari mwaka huu katika kituo cha Afya Murriet ambapo matibabu hayo yalikwenda sambamba na utoaji wa dawa na miwani bure kwa wagonjwa waliogundulika kuwa na matatizo ya macho yanayohitaji miwani.
Pichani: Moja ya wakazi wa kata ya Murriet akipokea ushauri wa daktari wa kituo cha Afya Murriet baada ya kufanyiwa vipimo vya presha na sukari wakati wa zoezi la uchunguzi na matibabu ya macho.
..............................................................................................................................................................................................................................
Akizungumza Wakati wa zoezi hilo Bw. Fazal Munisi ambaye ni mmoja ya wawakilishi wa Lions Club International alisema kuwa asilimia kubwa ya watu kwenye jamii hawajajiwekea utaratibu wa kupima afya ya macho mara kwa mara hali inayopelea madhara makubwa endapo mtu asipopata matibabu kwa wakati hivyo wameona ni vyema kujitolea huduma hiyo muhimu bila malipo kwa wananchi wa kata hizo mbili.
“Shukran zetu za dhati ziende kwa uongozi wa Mkoa wa Arusha kupitia kwa Mganga Mkuu wa Mkoa kwa kutupa kibali cha kuendesha zoezi hili katika kata hizi mbili za Jiji la Arusha ambapo hadi kufikia mwisho wa zoezi hili tunatarajia kutoa matibabu kwa zaidi ya wagonjwa 700”. alisema Bw. Munisi
Pichani: Watumishi wa kituo cha Afya Murriet wakiandikisha wananchi waliojitokeza katika zoezi la uchunguzi na matibabu ya macho.
................................................................................................................................................................................
Pia aliongeza kwa kuyataka mashirika na makampuni yasiyo ya kiserikali kujitolea kwa wingi kutoa huduma za afya kwa wananchi wa hali ya chini ambapo pia amebainisha kuwa licha ya matibabu hayo wanayotoa pia watagharamia gharama zote za upasuaji wa macho zitakazofanyika katika hospitali ya St. Elizabeth iliyopo Jijini Arusha pamoja na hospitali ya rufaa ya KCMC iliyopo wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro kwa wagonjwa waliofanyiwa vipimo katika zoezi hilo.
Pichani: baadhi ya wananchi waliogundulika na matatizo mbalimbali ya mamcho wakisubiri kuingia katika chumba cha dawa na miwani wakati wa zoezi hilo.
...........................................................................................................................................................................................................................................................................
Naye Mratibu wa afya ya macho Mkoa wa Arusha Bi. Mwanahawa Kombo alisema kuwa amefarijika na muitikio mkubwa wa watu katika zoezi hilo na amesema kuwa kundi kubwa linaloathirika zaidi na matatizo ya macho ni watu wenye umri wa miaka 60 na kuendelea na kundi jingine ni watoto wadogo kusumbuliwa na aleji zinazotokana na sababu mbalimbali.Zoezi hilo lililofanyika Tarehe 2-3 mwezi Februari mwaka huu katika kituo cha afya Murriet linatarajiwa kufanyika tena mwezi April mwaka huu kwa awamu ya pili huku vituo vya afya Kaloleni na Levolosi vikiendelea kutoa huduma ya uchunguzi na matibabu ya macho kama kawaida.
20 Boma Street 23101
Sanduku la Posta: 3013
Simu: 0272548072
Simu ya Mkononi: 0272545768
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa